Shaytwaan kujifananisha na umbile la Mtume kwenye kaburi

Swali: Je, shaytwaan anaweza kujifananisha na umbile la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwenye kaburi lake?

Jibu: Hata siku moja. Shaytwaan ajifananishe na umbile la Mtume? Ni jambo lisilowezekana. Lakini hata hivyo anaweza kuwadanganya wale wajinga na kuwaambia kuwa mimi ndio Mtume. Hili linawezekana. Ama kuhusu uhakika ni jambo haliwezekani akajifananisha na umbile la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Anachoweza ni kujifananisha na umbile lisilokuwa la Mtume na mtu ambaye sio msomi akamsadikisha kwa kuwa hajui umbile la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (13) http://alfawzan.af.org.sa/node/2128
  • Imechapishwa: 05/07/2020