Mgonjwa asiyeweza kwenda chooni kutawadha atafanya Tayammum?

Swali: Kuna mtu ni mgonjwa na hawezi kwenda chooni kutawadha. Ni ipi hukumu ya wudhuu´ wake? Je, afanye Tayammum pamoja na kuwa kuna uwezekano akaja mtu na maji na akamtawadhisha au inafaa kwake kufanya Tayammum?

Jibu: Ambaye hawezi kwenda chooni kutawadha anatakiwa kuletewa maji na atawadha mahali hapo alipo. Amesema (Tabaarak wa Ta´ala):

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

“Mcheni Allaah muwezavyo.” (64:16)

Ikiwa hawezi kuyafikia maji anaweza kuletewa maji na akatawadha kutoka kwenye maji hayo. Haijuzu kufanyia mchezo jambo hili.

Ama ikiwa ana  uzito katika kule kutia wudhuu´ wenyewe – ni mamoja ameyafuata maji hayo au ametawadha hapohapo alipo – hapo ndipo atatakiwa kufanya Tayammum.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (30) http://binothaimeen.net/content/694
  • Imechapishwa: 25/10/2017