Mgonjwa anayefanya Tayammum kwenye mto

Swali: Ni ipi hukumu ya swalah ya mwanamke mgonjwa anayefanya Tayammum kwenye mto na hafuniki nywele zake?

Jibu: Ikiwa mwanamke huyu hawezi zaidi ya aliyoyafanya; hawezi kushuka kitandani ili atawadhe au afanye Tayammum, na wala hawezi kufunika vile viungo anavyopaswa kufunika wakati wa kuswali, basi hakuna hana dhambi yoyote na swalah yake ni sahihi. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَاتَّقُوا اللَّـهَ مَا اسْتَطَعْتُمْ

”Mcheni Allaah muwezavyo.”[1]

لَا يُكَلِّفُ اللَّـهُ نَفْسًا إِلَّا وُسْعَهَا

“Allaah hakalifishi nafsi yoyote isipokuwa kwa kadiri ya uwezo wake.”[2]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ninayokukatazeni basi jiepusheni nayo na nikikuamrisheni jambo basi lifanyeni muwezavyo.”[3]

Lakini ikiwa anaweza kuyafanya yale mambo ya wajibu zaidi ya aliyoyafanya, basi haijuzu kwake kufanya hivo.

[1] 64:16

[2] 02:286

[3] al-Bukhaariy (7288) na Muslim (1337).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/299)
  • Imechapishwa: 02/08/2026