Hapa ndipo maamum wanatakiwa kuswali mkusanyiko ikiwa imamu hayupo

Swali: Kila wakati ninapotaka kukimu juu ya swalah ya Fajr kutokana na kukosekana kwa muda, waswaliji wananiomba kukaa chini mpaka imamu anipe idhini ya kukimu. Aidha wanasema kuwa haijuzu kukimu swalah mpaka imamu anipe idhini. Je, hayo ni sahihi?

Jibu: Muadhini ndiye mwenye haki zaidi ya adhaana. Yeye ndiye mwenye kumiliki adhaana. Kukimu imamu ndiye mwenye haki zaidi. Kwa hiyo muadhini asikimu isipokuwa mpaka ahudhurie imamu na baada ya idhini yake. Lakini pindi muda unapokuwa mfinyu kwa namna ya kwamba imamu akachelewa mpaka jua likakaribia kuzama, basi waswali na wasimsubiri. Lakini muda wa kuwa wakati bado upo basi wasiswali mpaka afike imamu. Hata hivyo imamu anatakiwa kuwawekea maamuma wakati maalum na kuwafahamisha maamuma kwamba akichelewa mpaka muda fulani basi wanatakiwa kuswali. Ni vyema kufanya hivo ili iwe rahisi na bora kwao na hivyo watu wasiingie ndani ya uzito.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/191-192)
  • Imechapishwa: 02/08/2026