Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia Siwaak baada ya alasiri ndani ya Ramadhaan?

Jibu: Hukumu yake ni kwamba hapana vibaya. Hukumu yake ni kwamba inapendeza katika hali zote katika nyakati zote. Inafaa kwa mfungaji na mtu mwengine kutumia Siwaak katika wakati wa alasiri na nyakati zingine. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

Siwaak inausafisha mdomo na inamridhisha Mola.”

“Lau nisingechelea kuwatia uzito ummah wangu basi ningewaamrisha Siwaak wakati wa kila swalah.”

Hili linaenea swalah ya Dhuhr, ´Aswr na nyenginezo kwa mfungaji na mtu mwingine.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/9280/حكم-السواك-بعد-العصر-في-رمضان
  • Imechapishwa: 29/03/2023