Swali: Kuna wenye kusema kuwa mfumo wa Salaf uliopo hii leo ni mfumo uliozushwa ambao umezushwa na baadhi ya watu kwa lengo la kuwajeruhi watu na kuwatoa katika Sunnah. Je, hili ni sahihi?
Jibu: Huu ni mgongano. Vipi itakuwa ni mfumo wa Salaf kisha uwe umezushwa? Salaf ni kitu kimetangulia; ni mfumo wa Maswahabah na wale wenye kuwafuata kwa wema. Huu ndio mfumo wa Salaf. Haukuzushwa. Yaliyozushwa ni yale yaliyokuja baada yake. Ama kuhusiana na mfumo wa Salaf ni wenye kuendelea. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Ummah huu utafarikiana katika mapote sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja.” Wakasema: “Ni kina nani hao?” Akasema: “Ni wale wataokuwa katika mfano wa yale niliyomo mimi hii leo na Maswahabah zangu.”
Yule ambaye anafuata katika yale aliyokuwemo Mtume na Maswahabah zake ndio mfumo wa Salaf. Haukuzushwa. Kilichozushwa ni maneno yake haya ya batili. Maneno haya ndio yamezushwa.
- Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13965
- Imechapishwa: 24/06/2020
Swali: Kuna wenye kusema kuwa mfumo wa Salaf uliopo hii leo ni mfumo uliozushwa ambao umezushwa na baadhi ya watu kwa lengo la kuwajeruhi watu na kuwatoa katika Sunnah. Je, hili ni sahihi?
Jibu: Huu ni mgongano. Vipi itakuwa ni mfumo wa Salaf kisha uwe umezushwa? Salaf ni kitu kimetangulia; ni mfumo wa Maswahabah na wale wenye kuwafuata kwa wema. Huu ndio mfumo wa Salaf. Haukuzushwa. Yaliyozushwa ni yale yaliyokuja baada yake. Ama kuhusiana na mfumo wa Salaf ni wenye kuendelea. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Ummah huu utafarikiana katika mapote sabini na tatu. Yote yataingia Motoni isipokuwa moja.” Wakasema: “Ni kina nani hao?” Akasema: “Ni wale wataokuwa katika mfano wa yale niliyomo mimi hii leo na Maswahabah zangu.”
Yule ambaye anafuata katika yale aliyokuwemo Mtume na Maswahabah zake ndio mfumo wa Salaf. Haukuzushwa. Kilichozushwa ni maneno yake haya ya batili. Maneno haya ndio yamezushwa.
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13965
Imechapishwa: 24/06/2020
https://firqatunnajia.com/mfumo-salaf-umezushwa-leo/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)