Mfuatiliaji huyu anaguswa na Hadiyth?

Swali: Ambaye anahudhuria darsa za kielimu kwa njia ya kuzisikiliza zinaporushwa moja kwa moja au anazisikiliza kwa njia ya intaneti anaingia katika maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hawatakusanyika watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Allaah… “?

Jibu: Hapana. Hawi kama wale waliokusanyika msikitini. Lakini anakuwa amechukua njia akitafuta elimu kwayo. Kuna njia nyingi za elimu ambapo baadhi ni bora kuliko zengine. Hili halina shaka yoyote. Kusema kuwa anatapa ujira kama yule ambaye anakaa msikitini ilihali hayuko msikitini si kweli.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (07) http://alfawzan.af.org.sa/node/2050
  • Imechapishwa: 26/12/2016