Mfano wa wanyama wasiofaa kuchinjwa katika ´Iydh-ul-Adhwhaa

Swali: Ni wanyama wepi ambao hawafai kuchinja katika ´Iyd-ul-Adhwhaa?

Jibu: Wanyama wanaofaa kuchinja ni wale wanyamahoa:

1 – Ngamia.

2 – Ng´ombe.

3 – Kondoo na mbuzi.

Kumewekwa sharti mwanamke huyo awe amesalimika na kasoro; asiwe chongo, mgonjwa, mnyonge na mwenye kusunda. Kondoo hasihi isipokuwa awe ametimiza miezi sita. Mbuzi hasihi isipokuwa awe ametimiza mwaka. Ng´ombe hasihi isipokuwa awe ametimiza miaka miwili. Ngamia hasihi isipokuwa awe ametimiza miaka tano.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (16875)
  • Imechapishwa: 19/07/2020