Swali: Nini maana ya kwamba shirki ndogo na kubwa na yenye kujificha na kidogo?
Jibu: Ni kwa namna yake ya dhahiri. Shirki ni aina mbalimbali. Shirki kubwa inajulikana, kama kuabudu masanamu, kuwa na mafungamano na mizimu, kuwaomba waliokufa na kuomba msaada kwa waliokufa. Haya yote ni shirki kubwa ya wazi.
Miongoni mwa shirki kuna aina ndogo. Ni yale yanayokuwa ndani ya nyoyo ikiwa ni pamoja na kujionyesha, kutafuta kusifiwa na watu na shukurani zao. Huenda mtu akaabudu, akaswali, akafunga au akasoma mbele ya watu na siri yake moyoni ni wapate kumsifu. Huenda akasoma kwa ajili hiyo, huenda akaenda sehemu fulani ili asifiwe kwa kwenda huko, kama vikao vya elimu au misikiti ya mbali ili aswali humo, si kwa ajili ya Allaah, bali ni kwa kutaka kujionyesha. Kwa hiyo shirki inakuwa katika mambo madogo sana ndani ya nyoyo, ambayo hayajulikani isipokuwa na Mjuzi wa yaliyofichika kutokana na aina za kujionyesha. Kwa ajili hii imekuja katika Hadiyth nyingine ya Abu Sa´iyd al-Khudwriy (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Je, nisikujulisheni kitu ninachokikhofia zaidi kwenu kwangu kuliko huyo al-Masiyh ad-Dajjaal?” Tukasema: ”Ndiyo, ee Mtume wa Allaah.” Akasema: ”Shirki yenye kujificha; mtu husimama akaswali, kisha akaipamba swalah yake kwa sababu ya kuona macho ya mtu yakimwangalia.”
Imekuja katika tamko jengine:
”Anayetafuta kusikiwa, basi Allaah atamfanya asikike. Na anayetafuta kujionyesha, basi Allaah atamfanya aonekane.”
Kwa kumalizia ni kwamba shirki kuna yenye kujificha na yenye kuonekana waziwazi, kidogo sana na kubwa sana. Shirki kidogo sana ni yale yanayokuwa ndani ya nyoyo, na yale yanayokuwa katika baadhi ya maneno ambayo watu hawatambui. Shirki ya wazi ni ile ambayo watu wanaiona na kuisikia, kama kuwaomba waliokufa, kuomba msaada kwa waliokufa, kutukana dini ya Uislamu, kuudhalilisha Uislamu na kuwatukana Mitume. Haya ni mambo ya wazi. Tunaomba Allaah atujaalie salama. Miongoni mwa mambo yenye kujificha ni yale yanayowachanganya watu, kama kusema ”Akitaka Allaah na akataka fulani”, ”lau sio Allaah na Mtume” au kuapa kwa amana. Haya hayatambuliki kwa baadhi ya watu na hawajui kuwa ni shirki. Kwa ajili hiyo hutokea sana katika maneno ya watu kuapa kwa asiye Allaah, kusema akitaka Allaah na akataka fulani, kutokana na ujinga wao na uchache wa elimu yao.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31682/ما-معنى-صغير-الشرك-وكبيره-وخفيه-ودقيقه
- Imechapishwa: 04/12/2025

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31682/ما-معنى-صغير-الشرك-وكبيره-وخفيه-ودقيقه
Imechapishwa: 04/12/2025
https://firqatunnajia.com/mfano-wa-shirki-kubwa-ndogo-na-yenye-kujificha/