Mchunga wanyama amefungua baada ya kuchoka kupindukia

Swali: Je, inafaa kwa mchunga ngamia, kondoo na mbuzi kufungua ikiwa amechoka kuchoka kukubwa na khaswa ikiwa anachunga wanyama hawa? Je, anapata ruhusa ya kufungua?

Jibu: Suala hili linahitaji upambanuzi. Ni lazima kwake kufunga ikiwa sio msafiri katika mji wala pembezoni mwa mji. Katika hali hiyo analazimika kufunga. Lakini ikiwa ni msafiri, basi inafaa kwake kula kama msafiri. Ama akiwa ni mkazi, hata hivyo hali imezidi kuwa mbaya zaidi kwa sababu ya uchungaji, jua na joto, huyu haifai kwake kufungua. Bali analazimika kuendelea kufunga. Isipokuwa ikiwa kama anachelea juu ya nafsi yake. Ikiwa ni dharurah na anakhofia khatari juu ya nafsi yake, basi inafaa kwake kufungua kwa sababu ya kuondosha madhara. Baada ya hapo ajizuilie siku iliyobaki. Kwa mfano kiu kikizidi ukali kiasi ambacho akachelea juu ya nafsi yake, atakunywa kisha atajizuilia. Baadaye atailipa siku hiyo kutokana na dharurah iliyomfika.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/15527/حكم-افطار-الراعي-لشدة-التعب
  • Imechapishwa: 25/03/2023