Madhehebu ya pili ni Shiy´ah na Raafidhwah ambao wanawachukia Maswahabah na wanawapenda watu wa nyumba ya kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Ahl-ul-Bayt, na wanapetuka mipaka kwao na wanavuka mipaka katika kuwapenda mpaka wakawaabudu pamoja na Allaah. Shiy´ah wako mapote zaidi ya ishirini. Katika hayo kuna mapote sita ya Zaydiyyah na Raafidhwah ni miongoni mwa Shiy´ah waliyopitiliza. Raafidhwah wanaonelea kuwa hakuna kupenda isipokuwa mpaka kupatikane kujitenga; bi maana kila anayedai kuwapenda Ahl-ul-Bayt basi madai yake hayasihi mpaka ajitenge mbali na Abu Bakr na ´Umar na watu wenye kuwawakilisha kama mfano wa ´Uthmaan na ´Aaishah.

Kuhusu madhehebu ya Shiy´ah, mbali na Raafidhwah, ni kuvuka mipaka kwa Ahl-ul-Bayt na wanaweza wasijitenge mbali na Maswahabah. Ama kuhusu Raafidhwah wao wanajitenga mbali na Maswahabah pamoja na kupetuka mipaka kwa Ahl-ul-Bayt. Baki ya Maswahabah wanajitenga nao mbali isipokuwa watu wachache kiasi cha watu kama kumi hivi nao ni wale ambao walisimama upande wa ´Aliy.

Wameitwa Raafidhwah kutokana na neno la kiarabu “kukataa/kujitenga.” Ni kwa sababu kusimama kwao upande wa Ahl-ul-Bayt na kuwakataa Maswahabah. Asli kuitwa kwao Raafidhwah ni kwa sababu ya kukataa/kujitenga na majlisi ya Zayd bin ´Aliy pindi alipokataa kumsema vibaya Abu Bakr na ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) .

Baina ya mayahudi, manaswara na Raafidhwah. Mayahudi na manaswara wamewapiku Raafidhwah katika nyanja moja nayo ni: Mayahudi waliulizwa ni watu wepi ambao ni bora katika dini yenu? Wakasema ni wanafunzi wa Muusa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Manaswara wakaulizwa ni watu wepi bora katika dini yenu? Wakasema ni wanafunzi wa ´Iysaa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Raafidhwah wakauliza ni watu wepi ambao ni waovu zaidi katika dini yenu? Wakasema ni Maswahabah wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hakuna wanaovuliwa humo isipokuwa idadi ya watu wachache ikiwa ni pamoja na ´Aliy na ´Ammaar. Miongoni mwa wale wanaowachafua kuko ambao ni bora kuliko wale waliowavua na wamewashinda na mbali kabisa. Mfano wa watu hao ni Abu Bakr, ´Umar na ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anhum).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (02/749-750)
  • Imechapishwa: 18/05/2020