Mawasiliano na watawala yanatakiwa kuwa kwa siri

Swali: Unasemaje juu ya mawasiliano ya moja kwa moja ya wanachuoni kwa watawala na khaswa hii leo kutokana na fitina inayoendelea katika miji. Wanachuoni wana mawasiliano ya moja kwa moja na watawala na wanawapa nasaha za moja kwa moja. Lakini ni kitu ambacho wakati mwingine hakidhihiri mbele ya watu wajinga na mbele za watu. Unaonaje juu ya njia kama hii?

Jibu: Ni kama ulivyosema. Ni wajibu kuwa na mawasiliano na watawala katika mambo yanayowahusu waislamu. Lakini hata hivyo hatuonyeshi kitu hichi. Hatusemi kuwa tumewasiliana nao na kuzungumza nao. Hatuonyeshi jambo hili. Ni siri.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Siyratiy adh-Dhaatiyyah http://www.alfawzan.af.org.sa/node/15901
  • Imechapishwa: 27/08/2020