Kwa yule anayetaka kuepuka fitina

Ni jambo lisilo na shaka kuwa Ummah hivi sasa unatembelea kwenye mawimbi ya fitina. Hili si geni. Ni jambo alilolielezea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu ya fitina itayopaitkana katika zama za mwisho. Pamoja na haya ametubashiria (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pale aliposema:

“Hakutoacha kuwepo kikundi katika Ummah wangu kuwa juu ya haki waziwazi. Hakitodhurika na wale wenye kuwakosesha nusura na wale wenye kwenda kinyume nao mpaka Qiyaamah kifike.”

Himdi zote ni za Allaah, hii ni bishara njema. Allaah anamuunga katika kikundi hichi yule anayemtakia kheri. Kipo na himdi zote ni za Allaah.

Jengine ni kuwa mtu hawezi kuepuka fitina na shari hizi mpaka pale atakaposoma ´Aqiydah. Akisoma ´Aqiydah kisawasawa atakuwa na asli ya kusimama juu yake na njia ya wazi anayotembelea. Hili khaswa khaswa kitabu “al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah” cha Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah. Kimefupisha madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na kimebainisha ´Aqiydah sahihi na misingi yao. Pamoja na kuwa ni kitabu kifupi ni chenye faida sana. Ni wajibu kukitilia umuhimu, kukihifadhi na kukisoma chini ya wanachuoni wataomfafanulia nacho. Humo (Rahimahu Allaah) ameandika njia ya wazi kwa wale wataokuja baada yake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Muhadhara: Siyratiy adh-Dhaatiyyah http://www.alfawzan.af.org.sa/node/15901
  • Imechapishwa: 27/08/2020