Swali: Wakati ninapokumbuka kaburi, mauti na mawaidha makali, hupatwa madhara au udhaifu. Wakati mwingine huenda napatwa na ugonjwa wa mwili na kwenda hospitali na hupata wasiwasi ndani ya nafsi yangu, jambo linalonifanya nijitenge na baadhi ya mawaidha. Ni yepi maoni yako juu ya hilo?

Jibu: Hii ni kheri kwako; kwamba unaathirika na mawaidha, hata kama yanaleta ugonjwa, usijitenge nayo. Jiandae kwa Aakhirah na pambana dhidi ya nafsi yako mpaka uwe na nguvu ya kupokea mawaidha bila kuathirika kwa athari inayokudhuru. Hakika Salaf walikuwa wanaathirika. Kiasi cha kwamba ´Umar alikuwa wakati mwingine akisikia Aayah kutoka Kitabu cha Allaah, huugua kwa sababu ya athari yake kubwa. Vilevile wengineo miongoni mwa waja wema na watu wema wanaposikia mawaidha na Aayah za Qur-aan au wanapozisoma usiku wakati mwingine, huathirika nazo. Kwa hiyo una mfano kwao, ee ndugu yangu, una ruwaza njema.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3263/حكم-من-تاثر-وتضرر-بسماع-المواعظ-البليغة
  • Imechapishwa: 06/08/2026