Swali: Tunaomba ubainishe usahihi wa Hadiyth hizi:
“Dini ni muamala.”
“Chagueni kwa mbegu zenu kwani asili huathiri.”
“Muumini hupenda na hupendwa. Hakuna kheri kwa asiyependa wala kupendwa.”?
Jibu: Maneno:
”Dini ni muamala.”
si Hadiyth, bali ni maneno ya watu. Hadiyth iliyo Swahiyh ni ile isemaayo:
“Dini ni kupeana nasaha.”
Ama maneno:
“Dini ni muamala.”
si katika Hadiyth.
Ama Hadiyth:
“Chagueni kwa mbegu zenu…”
hii si sahihi. Bali ni katika Hadiyth dhaifu ambazo hazitegemewi. Hata hivyo maana yake ni sahihi. Kwa maana mtu anatakiwa achague mke au mume mwenye dini njema, kheri na tabia nzuri.
Kuhusu maneno yasemayo:
“Muumini hupenda na hupendwa. Hakuna kheri kwa asiyependa wala kupendwa.”
sijui usahihi wake na wala sijui hali ya cheni yake ya wapokezi. Sijui daraja yake; itachunguzwa – Allaah akitaka. Itaelezwa hali yake baadaye – Allaah akitaka.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3211/درجة-حديث-الدين-المعاملة-وحديث-تخيروا-لنطفكم
- Imechapishwa: 06/08/2026
Swali: Tunaomba ubainishe usahihi wa Hadiyth hizi:
“Dini ni muamala.”
“Chagueni kwa mbegu zenu kwani asili huathiri.”
“Muumini hupenda na hupendwa. Hakuna kheri kwa asiyependa wala kupendwa.”?
Jibu: Maneno:
”Dini ni muamala.”
si Hadiyth, bali ni maneno ya watu. Hadiyth iliyo Swahiyh ni ile isemaayo:
“Dini ni kupeana nasaha.”
Ama maneno:
“Dini ni muamala.”
si katika Hadiyth.
Ama Hadiyth:
“Chagueni kwa mbegu zenu…”
hii si sahihi. Bali ni katika Hadiyth dhaifu ambazo hazitegemewi. Hata hivyo maana yake ni sahihi. Kwa maana mtu anatakiwa achague mke au mume mwenye dini njema, kheri na tabia nzuri.
Kuhusu maneno yasemayo:
“Muumini hupenda na hupendwa. Hakuna kheri kwa asiyependa wala kupendwa.”
sijui usahihi wake na wala sijui hali ya cheni yake ya wapokezi. Sijui daraja yake; itachunguzwa – Allaah akitaka. Itaelezwa hali yake baadaye – Allaah akitaka.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3211/درجة-حديث-الدين-المعاملة-وحديث-تخيروا-لنطفكم
Imechapishwa: 06/08/2026
https://firqatunnajia.com/hadiyth-zote-hizi-ni-dhaifu/