Swali: Katika Hijjah ya mwaka huu nilirusha vijiwe siku ya pili na ya tatu, nikianza na jiwe kubwa, kisha la kati, kisha la kwanza, kwa maana nyingine niligeuza mpangilio wa kurusha. Je, nina wajibu wa kuchinja Hadiy au kutoa fidia?

Jibu: Hapana. Jambo hili lina makinzano baina ya wanazuoni na Sunnah ni kuanza na lile lililoko Minaa karibu na msikiti wa Khayf, kama alivyoanza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kisha ashuke kuelekea Makkah, arushe la kati, kisha la mwisho ambalo ni Jamrat-ul-´Aqabah, ambalo alilirusha siku ya ´iyd. Hilo linakuwa la mwisho katika siku za Tashriyq. Kufanya hivi ndiyo Sunnah. Lakini ikiwa amegeuza, basi afundishwe. Ikiwa bado yuko katika wakati wa kurusha, akigeuza anarudi na kurusha la kati, kisha la mwisho ili liwe baada ya la kwanza. Lakini kwa kuwa wakati umepita, inamtosheleza – Allaah akitaka. Kwa sababu makinzano yapo na jambo ni lenye wasaa. Maadamu wakati umepita na tayari amerusha, basi himdi zote ni za Allaah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3257/حكم-عكس-الرمي-في-الحج
  • Imechapishwa: 06/08/2026