Swali: Mama yangu amenitaka nimpe msichana wanug jina analolipenda yeye, nalo ni jina la mama yake, na mimi nataka nimpe jina la mmoja wa mama wa waumini au Maswahabah wa kike. Naomba fatwa, je, nitekeleze matakwa ya mama yangu?

Jibu: Ndiyo, matakwa ya mama yako ni ya kwanza kabla ya matakwa yako. Ikiwa jina alilolitaja mama yako halina jambo lililokatazwa. Hapo ni pale amnbapo ikiwa ni jina linaloruhusiwa na halina tatizo, mfano amesema anataka aitwe Maryam na wewe unataka aitwe Faatwimah au ´Aaishah, basi mpe kipaumbele mama. Majina yote hayo yanafaa. Katika kutanguliza alichosema mama yako kuna kheri nyingi na kuridhika kwake, na jambo hili ni ni lenye wasaa. Kwa ahivyo hakuna haja ya kumuasi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3277/طاعة-الام-في-تسميتها-المولود
  • Imechapishwa: 06/08/2026