Maulidi yalianza baada ya karne tatu bora

Swali: Maulidi ulianza lini? Je, ilidhibitiwa tarehe ambayo tukio la maulidi lilitokea? Je, kumeandikwa vitabu ambavyo vinaweza kufaidika navyo katika mada hii?

Jibu: Maulidi kwa uhakika haijulikani yalianza lini hasa. Lakini kwa yakini yalianza baada ya karne tatu. Wanazuoni wametaja kwamba hakuna chochote katika hilo kilichotokea isipokuwa baada ya karne tatu zilizofadhilishwa. Lililo mashuhuri ni kwamba lilitokea katika zama za mfalme wa Irbil, al-Malik al-Mudhwafar, Abu Sa´iyd, mwishoni mwa karne ya sita au mwanzoni mwa karne ya saba, kwa sababu alikufa mwaka thelathini na mia sita. Baadhi ya wanahistoria, kama mtunzi wa kitabu ”al-Ibdaa´ fiy Madhwaar al-Ibtidaa´”, ametaja kwamba amesema baadhi yao:

”Ilionekana pia katika karne ya nne kwa mkono wa Faatwimiyyah, wafalme wa Misri na Moroco. Walianzisha maulidi tano katika karne ya nne: mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Faatwimah, al-Husayn, al-Hasan na mengine kwa ajili ya mfalme wao, khalifah wao.”

Kwa hali yoyote ile kusherehekea maulidi kulitokea tu baada ya karne bora. Lililo mashuhuri ni kwamba lilitokea baada ya karne sita katika zama za al-Malik al-Mudhwafar Abu Sa´iyd, mwishoni mwa karne ya sita na mwanzoni mwa ya saba katika Irbil.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1653/زمن-ظهور-بدعة-الاحتفال-بالمولد
  • Imechapishwa: 13/08/2026