Msimamo kwa mtoto ambaye wazazi wake hawataki afunge

Swali: Ni ipi hukumu ikiwa mtu amefunga siku swawm ya masiku meupe na katika wakati wa kufunga mzazi mmoja akaapa kwamba avunje funga. Je, avunje funga au aendelee na swawm yake?

Jibu: Kuwafanyia wema wazazi ni wajibu na kufunga masiku meupe ni jambo la kusuniwa, hivyo haifai kutanguliza jambo la kusuniwa juu ya la wajibu. Ikiwa wazazi wake wanamwonea huruma na wanamkhofia kwa sababu ya joto kali, kitu kinachofanana na hicho au kwa sababu anatelekeza mambo yanayowanufaisha, anatelekeza wanayoyahitaji katika mahitaji ya nyumba kama kuuza, kununua, kulima au kazi za shambani na mambo mfano wa hayo na wao ni wenye kuhitajia jambo hilo. Makusudio ni kwamba ikiwa nia yao ni kheri na ni nzuri, basi awajibu wazazi wake na asifunge swawm ya kujitolea. Kwa sababu swawm ya kujitolea ni jambo la linalopendeza na kuwafanyia wema wazazi ni jambo la wajibu, na wajibu unatangulizwa juu ya jambo la kusuniwa.

Swali: Vipi ikiwa makusudio yao ni huruma tu kwa mtoto?

Jibu: Haijalishi kitu, ikiwa kufunga kunawatia dhiki na huenda kukawapelekea kumkataza au kuwakasirisha, basi na amche Allaah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1356/حكم-طاعة-الوالدين-في-ترك-اعمال-مستحبة
  • Imechapishwa: 13/08/2026