Swali: Ahl-us-Sunnah wamekosolewa sana juu ya msimamo wao kwa watawala na maandamano mpaka imesemekana kwamba Ahl-us-Sunnah ndio ngao ya kinga kwa watawala. Tunataraji utuwekee wazi na nasaha juu ya jambo hili?

Jibu: Ahl-us-Sunnah ni ngao ya kinga dhidi ya ghasia na matatizo. Baada ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Ahl-us-Sunnah ndio ngao ya kinga dhidi ya mapinduzi, migomo, fujo, fitina na matatizo. Chukueni mafunzo kwa wengine! Kwa mfano Somalia. Tokea lini wana ghasia, fitina, matatizo, mauaji na vita? Mpaka hivi leo bado yanaendelea na Allaah ndiye Anajua zaidi mpaka lini yataendelea.

Ndugu! Ahl-us-Sunnah ni watu wameshikamana na elimu, ufahamu, Baswiyrah, uzowefu na subira. Wanalinganisha manufaa na madhara. Wanajumuisha baina ya dalili za Kishari´ah na wanazitendea kazi katika maisha yao. Maandamano haya hayakuchangia zaidi isopokuwa fitina za visa, chuki, mauaji, vita, matatizo na ghasia. Jitahidini na amani! Jitahidini na amani, utulivu, maelewano na subira na kuweni pamoja na wanachuoni. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Sikilizeni na mtii hata kama atakupiga mgongo wako na kuchukua mali yako.”

Sikiliza na utii! Subiri. Subiri na wala usijivue katika utiifu wa mtawala Muislamu hata kama atakuwa ni mkandamizaji na mjeuri. Kwa kuwa kumfanyia uasi sio jambo rahisi. Linasababisha matatizo, fitina na vita. Tendea kazi yaliyokuja kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na unabashiriwa kheri. Tendea kazi Qur-aan na Sunnah. Je, Qur-aan na Sunnah vinaamrisha ghasia, matatizo na uasi dhidi ya watawala wa Waisamu? Hapana. Kinyume chake.

Ghasia hizi zimekuja kutoka kwa makafiri. Mudiri yeyote wa idara fulani, raisi, kiongozi au raisi wasiyompenda, wanatoka nje na kuadamana. Wanamjeruhi na wanataka aache kazi yake. Hili hufanywa na kakundi ka vijana, watoto na wale wasiokuwa na kazi ndio wanatoka nje wakipiga fujo na kutukana. Je, kweli hii ndio njia ya Shari´ah? Wanamuona mtawala kwao kama mtu wa kawaida tu asiyekuwa na hadhi yoyote wala fadhila? Ndugu zangu! Hii ni vurugu. Haya ndio matunda ya wanademokrasia. Ghasia, fitina, matatizo, uasi dhidi ya mtawala, mauaji, vita na uhuru kwa kutumia jina la uhuru na jina la demokrasia ni matunda ya wanademokrasia. Waambie:

“Hivi sasa okota matunda safi ya demokrasia; kwa ghasia inyofanywa usiku na mchana.”

Ahl-us-Sunnah ni walinganiaji wa amani na usalama. Wanalingania katika Tawhiyd, ´Aqiydah, ´ibaadah, swalah, Istiqaamah na subira. Kuweni na subira kwa mtawala hata kama atakuwa ni mkandamizaji:

إِنَّمَا يُوَفَّى الصَّابِرُونَ أَجْرَهُم بِغَيْرِ حِسَابٍ

“Hakika wanaosubiri watalipwa kikamilifu ujira wao bila ya hesabu.” (39:10)

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab al-Waswaabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.ibnbaz.se/Artiklarna/301-400/059.html
  • Imechapishwa: 05/09/2020