Mwenye kufa katika maandamano ni shahidi?

Swali: Sauti si nzuri na kitu tumechoweza kusikia katika swali ni hukumu ya maandamano kwa idhini ya kanuni pamoja na mwandamaji mwenye kufa katika maandamano…

Jibu: Huyu amekufa katika fitina. Ama kwamba ni shahidi, Allaah ndiye anajua zaidi. Sisi hatuwezi kuhukumu kuwa ni shahidi isipokuwa yule aliyeshuhudiwa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hata hivyo amekatazwa kufanya hivyo. Hapati kushiriki katika maandamano. Yeye ndiye amesababisha kuiua nafsi yake. Allaah ndiye Mwenye kujua yatayopitika naye na mafikio yake. Amekosea. Yeye mwenyewe ndio amejisababishia kuuawa na yaliyomfika.

Shari´ah haijuzishi maandamano. Shari´ah ya Uislamu haijuzishi maandamano. Ama kanuni za baadhi ya nchi kuyajuzisha, mtu anatakiwa kujua kwamba kanuni ni batili. Ni kanuni za kikafiri. Hazitumiwi kama dalili wala hoja. Dalili yetu ni Shari´ah na sio kanuni. Dalili ya muislamu ni Shari´ah na sio kanuni za Kishaytwaan.

Check Also

Pale ambapo maandamano yanapelekea katika madhara makubwa zaidi

Kwanza ikiwa mtawala ni muislamu na hajatoka katika Uislamu, haijuzu kabisa kumfanya uasi. Atafanyiwa subira. …