Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hufunguliwa milango ya Pepo siku ya jumatatu na siku ya alkhamisi. Hivyo akasamehewa kila mja asiyemshirikisha Allaah na chochote; isipokuwa watu wawili ambao kati yake yeye na ndugu yake kuna magomvi. Kunasemwa: “Wasubirini hawa wawili hadi wapatane. Wasubirini hawa wawili hadi wapatane. Wasubirini hawa wawili hadi wapatane.”

Je, ni madhambi madogo ndio yanayosamehewa?

Jibu: Kwa mujibu wa Aayah:

إِنَّ اللَّـهَ لَا يَغْفِرُ أَن يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَاءُ

“Hakikaha hasamehi kushirikishwa na anasamehe yaliyo chini ya hayo kwa Amtakae.”[1]

Ikiwa ni kwa kutubia madhambi yote yanasamehewa ya kila mja asiyemshirikisha Allaah na chochote. Hapa kuna ahadi na matarajio kwa watenda madhambi. Hata hivyo zipo Hadiyth na Aayah nyengine zilizofahamisha kuwa kudumu juu ya madhambi makubwa ni miongoni mwa sababu za kutokusamehewa.

Swali: Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“… asiyemshirikisha Allaah na chochote.”

Jibu: Ni yenye kuenea na kunaingia aina zote mbili.

[1] 04:48

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23442/معنى-حديث-يغفر-لكل-عبد-لا-يشرك
  • Imechapishwa: 20/01/2024