Matembezi na kuswali maeneo ambapo waliadhibiwa wapinzani wa Mitume

Swali: Je, hukumu inakuwa sawa ikiwa kunatokea kudidimizwa katika baadhi ya miji baada ya Mitume?

Jibu: Udhahiri ni kwamba [makatazo] ni yenye kuenea. Hawa ni wenye kuadhibiwa, kama alivosema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Msiingie kwa hawa walioadhibiwa mkaja kufikwa na yale yaliyowafika.”

Tunamuomba Allaah usalama. Mtu anatakiwa kujiweka mbali na maeneo hayo na aswali sehemu nyingine.

Swali: Ni kwa njia ya kuchukiza?

Jibu: Udhahiri wa makatazo ni haramu. Makusudio yake hapa ni uharamu. Haya ndio makusudio yake.

Swali: Hakukisiwi kiwango cha uharamu yaliyoachiwa kutokana na yale yaliyopokelewa kutoka kwa Salaf?

Jibu: Kulingana na dalili.

Swali: Swalah inasihi?

Jibu: Udhahiri wa makatazo ni uharamu na hivyo haisihi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23626/حكم-الدخول-على-من-خسف-بهم-بعد-الانبياء
  • Imechapishwa: 02/03/2024