Swali: Je, mate yanafunguza katika Ramadhaan kwa vile hukusanyikiwa na mate mengi khaswa khaswa ikiwa nasoma Qur-aan na msikitini?

Jibu: Mfungaji kumeza mate hakuharibu swawm yake. Haijalishi kitu hata kama hilo litatokea kwa wingi na mara kwa mara msikitini na kwenginepo. Lakini ikiwa yamefikia kiwango cha makohozi usiyameze. Yateme kwenye kitambaa au kitu mfano wake ikiwa uko msikitini.

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (10/270)
  • Imechapishwa: 11/06/2017