Swali: Vipi kuhusu baadhi ya mihadhara inayofanywa na baadhi ya al-Ikhwaan. Wanasema mfumo wa Salaf katika tabia na mfumo wa Salaf katika ´Aqiydah. Baadhi ya wanaofanya mihadhara hii ni katika al-Ikhwaan al-Muslimuun.

al-Madkhaliy: Wanasema mfumo wa Salaf?

Muulizaji: Ndio. Wanasema mfumo wa Salaf ilihali wao wako mbali kabisa na mfumo wa Salaf.

al-Madkhaliy: Wako mbali na mfumo wa Salaf na ulinganizi wao juu ya vijana wa Ummah ni mbaya  sana. Wanaipamba kwa kutumia neno´Salaf`. Vingienevyo hawatowakubalia.

Ni lazima kwa watu kuzinduka juu ya hadaa hii. Ninaapa kwa Allaah kwamba hatujawaona watu ambao wana madhara na khatari zaidi juu ya mfumo wa Salaf. Wao hivi sasa wanajificha nyuma ya al-Albaaniy, Ibn Baaz, Ibn ´Uthaymiyn, Ibn Taymiyyah na nyuma Ibn ´Abdil-Wahhaab. Kwa sababu Da´wah ya Sayyid Qutwub, al-Bannaa na al-Mawduudiy haiwezi kutembea kati ya wenye busara. Matokeo yake wanajificha nyuma ya watu hawa kwa lengo la kuwadanganya watu. Sisi hatuhitajii kusema yale yaliyosemwa al-Bannaa na al-Mawduudiy. Bali tunanukuu yale yaliyosemwa, Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), tunachukua yale maneno ya maimamu wa Kiislamu yaliyowafikiana na Qur-aan na Sunnah.

Nasaha zangu kwa waislamu watahadhari juu ya watu hawa na waelewe. Nasaha zangu juu ya watu hawa wamche Allaah, wasome mfumo wa Salaf wa kweli, wazilee nafsi zao juu yake na wawalee watoto wa Ummah juu ya mfumo huu ambao hii leo uko wazi kabisa kama jua linavoonekana. Vitabu vipo na vimetangaa kuhusu ´Aqiydah, ´ibaadah, mfumo na mengineyo yote. Ni lazima kwao wamche Allaah, waache ukaidi, kiburi na kushikamana na fikira za al-Bannaa, al-Mawduudiy na Sayyid Qutwub ambao ni watu wa Bid´ah na wapotevu. Kwani mfumo wa Salaf haikutani kabisa na mifumo ya watu hawa isipokuwa tu katika baadhi ya mambo.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa fiyl-´Aqiydah wal-Manhaj al-Halaqah ath-Thaaniy http://www.rabee.net/ar/questions.php?cat=31&id=657
  • Imechapishwa: 20/01/2019