Swali: Kuna kaseti zinazouzwa ambazo zimerekodiwa Aayah za matabano. Je, njia hii imewekwa katika Shari´ah na inatosheleza?

Jibu: Haijuzu kuziuza kwa njia hii. Matabano yanakuwa moja kwa moja kutoka kwa yule msomaji kwenda kwa yule anayesomewa ambapo anamtemea cheche za mate. Ama kurekodi kwenye kaseti na mfano wake si sawa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (31)
  • Imechapishwa: 26/02/2022