Mashindano pekee ambayo inafaa kuwekeana dau

Swali: Vipi kuhusu kubashiriana kati ya watu wawili?

Jibu: Kubashiriana ni kamari; isipokuwa katika mashindano ya ngamia, farasi au upigaji mishale. Ama kubashiriana kwa kusema “Ikiwa itakuwa hivi, basi nitakupa hivi, na ikiwa itakuwa vinginevyo, basi nitakupa hivi”, basi hiyo ni kamari na haifai. Kubashiriana hufanyika kati ya watu wawili au zaidi kwa njia ya kushiriki, ambayo inamaanisha ni kati ya wawili.

Swali: Je, inajuzu kwa watu wawili kufanya mashindano ya farasi kwa masharti ya kila mmoja kuweka pesa?

Jibu: Ndiyo, wanaruhusiwa kusema “Tutashindana mimi na wewe” kisha kila mmoja atoe kiasi fulani – kama elfu moja au elfu mbili – na mshindi achukue yote. Hili ni sahihi na halina tatizo, kwani linasaidia kujifunza na kufundisha farasi wao kwa ajili ya mashindano.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25427/ما-كيفية-المراهنة-والمسابقة-الجاىزة
  • Imechapishwa: 24/03/2025