Mashindano ambayo washindi wamewekewa zawadi na dau

Swali: Vikundi vitano vimekusanyika, kila kikundi kimechangia 1000 SAR na kuweka jumla ya 5000 SAR kwa mshindi kati yao. Ikiwa mmoja wao atashinda kwenye mpira kikundi chake kinaruhusiwa kuchukua pesa hizo?

Jibu: Hili halijuzu. Michezo ya mpira au mingine yoyote haipaswi kuwa na dau la fedha au zawadi za kifedha, isipokuwa kwa mashindano matatu tu:

1 – Mashindano ya upigaji mishale.

2 –  Mashindano ya ngamia.

3 –  Mashindano ya farasi.

Yasiyokuwa haya haijuzu kuwepo dau au zawadi. Hapana vibaya wakashindana kwa kukimbia kwa miguu, lakini bila kuweka dau. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna dau au zawadi isipokuwa kwa [mashindano ya] mishale, ngamia au farasi.”

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24972/حكم-الالعاب-التي-يكون-فيها-عوض
  • Imechapishwa: 16/01/2025