Swali: Mtoto wangu anataka kusafiri kwenda Malaysia kwa ajili ya Da´wah. Unamnasihi kwenda?

Jibu: Ikiwa yuko na elimu basi anaweza kwenda Malaysia na kwengine na kulingania katika dini ya Allaah. Ikiwa hana elimu asisafiri. Hatakiwi vilevile kusafiri ikiwa ameshikamana na mfumo wa kupinda ambao analingania kwao. Ni lazima kwake kulingania katika mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ikiwa yuko na elimu juu yake. Ikiwa yuko na elimu juu ya mfumo wa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni jambo zuri akalingania kwao. Hata hivyo hatakiwi kulingania katika mfumo wa mtu au wa kundi fulani. Katika hali hiyo haijalishi kitu sawa ikiwa ni katika nchi ya Kiislamu au nchi ya kikafiri. Haijuzu kulingania katika makundi na mifumo inayoenda kinyume na mfumo wa Salaf pasi na kujali popote pale mtu alipo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (24) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsir-ayat-qrran-19-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 20/06/2020