Mashambulizi ya Redio ya London kwa Ibn Baaz

Swali: Leo redio ya London imezungumza kuhusu yale mliyoyaandika na wakakushambulia kwa mashambulizi mabaya na ya aibu. Tunaomba majibu ili kubatilisha shubuha zao.

Jibu: Nimesikia kwamba wametangaza yale tuliyoandika kuhusu kukataza kusafiri kwenda katika nchi za washirikina. Hakika hilo linawaudhi, kwa sababu wanapenda wana wetu na wanafunzi wetu waende kwao ili wawaharibie dini yao na wachukue mali zao. Hivyo kwenda kwa vijana wetu huko kuna manufaa kwao:

1 – Kuchukua mali zao.

2 – Kuharibu dini yao.

Kwa hiyo wakisikia mtu anayezungumza kuhusu kuzuia kusafiri, hapana shaka watatukana na watakasirika. Lakini hasira yao inatufaa wala haitudhuru. Allaah awazidishie shari na hasira.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2457/تعليق-على-ما-نشرته-اذاعة-لندن-حول-منع-السفر-الى-بلاد-الكفر
  • Imechapishwa: 29/03/2026