Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuwa Ummah huu utagawanyika makundi sabini na tatu. Je, haya makundi ya Kiislamu yanayojulikana, kama mfano wa al-Ikhwaan, Jamaa´at-ud-Da´wah na Jamaa´at-u-Islaamiyyah wal-Jihaad ni katika mapote yaliyoangamia?

Jibu: Jambo la kwanza makundi yote haya yamezushwa. Jamaa´at-ut-Tabliygh ni kundi lililozushwa. al-Ikhwaan al-Muslimuun ni kundi lililozushwa. Kundi lililowekwa katika Shari´ah ni lile alilosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), wakati alipoulizwa juu ya kundi lililookolewa na kunusuriwa, akasema:

“Ni lile litakalokuwa juu ya yale niliyomo mimi hivi leo na Maswahabah zangu.”

Yule atakayeangalia mifumo ya makundi haya, kama mfano wa Jamaa´at-ut-Tabliygh au al-Ikhwaan, ataona kuwa wanaenda kinyume katika mambo yao mengi ya ´Aqiydah na matendo yao. Makundi haya yametumbukia katika mambo mengi ya Bid´ah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amehukumu kuwa Bid´ah ni upotevu na akawatisha watu wake na Moto pale aliposema:

“Hakika kila ya Bid´ah ni upotevu na kila upotevu ni Motoni.”

Kila siku tunatahadharisha kundi la Jamaa´at-ut-Tabliygh na kundi la al-Ikhwaan baada ya kujua mifumo na madhehebu yao ambayo wametahadharisha wanachuoni waaminifu. Kuna wanachuoni wengi wametahadharisha na sio idadi ya watu wachache kutokana na upotevu unaopatikana katika mifumo yao unaoenda kinyume na njia iliyonyooka. Sisi tunatahadharisha mapote haya. Wala hayazingatiwi kuwa ni makundi, kwa sababu kundi ni limoja tu. Nalo si lengine ni lile alilosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) juu yake:

“Ni Jamaa´ah.”

Mapote haya yameenda kinyume na mfumo wa kundi ambalo linafuata Qur-aan na Sunnah katika mambo yao mengi ya ´Aqiydah, matendo na mfumo wao.

Ni juu ya kila Muislamu mwanaume na mwanamke atahadhari nayo. Makundi haya ndio sababu ya mfarakano.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=27686
  • Imechapishwa: 11/04/2015