Maoni ya wanazuoni kuhusu Aayah ya kumlazimisha mtu kuingia dini

Swali: Aayah isemayo:

لَا إِكْرَاهَ فِي الدِّينِ

“Hapana kulazimisha katika dini.”[1]

ni yenye kufuatwa na Aayah ya upanga?

Jibu: Wengine wamesema imefutwa na wengine wamesema kuwa inawahusu watu wa Kitabu pekee. Wanazuoni wana mitazamo miwili:

1 – Inawahusu watu waliopewa Kitabu na waabudia moto. Hawa hawalazimishwi, bali wanapewa chaguo kati ya Uislamu na kulipa kodi. Wakiwa hawakulipa kodi wala kuingia katika Uislamu, basi wanapigwa vita. Ama watu wengine waliobaki, hawana chaguo; ni Uislamu au upanga.

2 – Wengine wamesema kuwa imefutwa. Hii ilikuwa katika mwanzo wa Uislamu, kisha Allaah akapanga vita na jihaad. Amesema (Subhaanahu wa Ta´ala):

وَقَاتِلُوهُمْ حَتَّىٰ لَا تَكُونَ فِتْنَةٌ وَيَكُونَ الدِّينُ كُلُّهُ لِلَّـهِ

“Na piganeni nao mpaka kusiweko fitina na dini yote iwe kwa ajili ya Allaah.”[2]

Kwa hiyo imefutwa kwa Aayah hii na zilizo na maana yake.

[1] 02:256

[2] 08:39

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31487/هل-نسخت-اية-السيف-اية-لا-اكراه-في-الدين
  • Imechapishwa: 25/10/2025