Manukato yanapoingia kwenye nguo za Ihraam

Swali: Je, manukato yanapaswa kuwekwa kwenye nguo za Ihraam au mwilini?

Jibu: Manukato yanapaswa kuwekwa mwilini, siyo kwenye nguo za Ihraam. Manukato huwekwa mwilini kama vile kichwani na ndevu.

Swali: Je, ni lazima kuosha manukato yaliyowekwa mwilini iwapo yatafika kwenye nguo za Ihraam au yanasamehewa?

Jibu: Jambo lililo karibu zaidi ni kuyasafisha. Ikiwezekana kuyasafisha, kufanya hivyo ni bora na ni salama zaidi kwa mujibu wa Hadiyth inayosema:

“Msivae chochote kilichoguswa na zafarani au Wars [aina ya manukato].”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24952/حكم-زي-الاحرام-اذا-اصابه-شيء-من-طيب-البدن
  • Imechapishwa: 11/01/2025