Anayefanya ´Umrah katika Ramadhaan na akabaki mpaka wakati wa Hijjah

Swali: Je, maneno ya Shaykh-ul-Islaam kwamba mtu anayefanya ´Umrah ya peke yake katika Ramadhaan na kubaki Makkah mpaka Hijjah ni bora kuliko yule anayefanya Tamattu’ wakati wa Hijjah. Je, ni sahihi?

Jibu: Hili ni eneo lenye nafasi ya kuzingatia. Jambo ni lenye wasaa. Ikiwa mtu atafanya ´Umrah katika Ramadhaan na kubaki mpaka ahiramie kwa ajili ya Hijjah hakuna tatizo. Na ikiwa anataka kuchukua ´Umrah katika miezi ya Hijjah, pia hakuna tatizo. Lakini makusudio yanayozungumziwa katika Hadiyth ni pale mtu anapokuja kufanya ´Umrah katika miezi ya Hijjah – hili ndilo eneo la kuzingatia. Ama yule anayefika katika Ramadhaan, Sunnah ni ahiramie kwa ´Umrah peke yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24954/حكم-من-اعتمر-في-رمضان-وبقي-الى-الحج
  • Imechapishwa: 11/01/2025