Maneno ya Mtume yanatangulia kablaa ya kitendo cha ´Aaishah

Swali: Ni ipi hukumu ya wanawake kuyatembelea makaburi? Je, imepokelewa ya kwamba ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) alitembelea kaburi la kaka yake?

Jibu: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah amewalaani wanawake wenye kuyatembelea makaburi na wale kuyafanya ni sehemu ya kuswalia na kuyawekea mataa.”[1]

Kwa hivyo haijuzu kwa mwanamke kuyatembelea makaburi. Kamwe. Kitendo cha ´Aaishah kutembelea kaburi la kaka yake ni kitendo cha Swahabah kisichoangusha Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

[1] Imethibiti kwa mujibu wa Ibn Taymiyyah katika ”Madjmuu´-ul-Fataawaa” (31/206).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (58) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/15-01-1438-ighastat.mp3
  • Imechapishwa: 22/10/2017