Swali: Maneno yaliyopokelewa ya Salaf kuhusu Tafsiyr ya Qur-aan yakubaliwe bila ya kufanya utafiti wa mlolongo wa wapokezi au ni lazima kufanya utafiti wa mlolongo wa wapokezi unaofikisha kwa watu waliyoyasema?

Jibu: Ee ndugu! Wanachuoni waliobobea wameandika mapokezi haya na maneno haya na wanaaminika. Wanaaminika na himdi zote ni za Allaah kwa kuwa wana elimu kubwa usiokuwa nayo wewe. Inatosheleza kwako kuwaiga na kustafidi na maneno yao pasina kuwa na mashaka juu ya hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (25) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1428-3-28.mp3
  • Imechapishwa: 19/08/2020