Maneno aliyopindisha al-Hajuuriy akidai kuwa al-Waadi´iy anaafikiana na mtazamo wake wa makosa

Shaykh na Muhaddith Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy (Rahimahu Allaah) amesema katika “Riyaadh-ul-Jannah” (23):

“Watu walio karibu zaidi ambao wanaendana na sifa hizi ni Ahl-ul-Hadiyth. Amesema zaidi ya mwanachuoni mmoja ya kwamba makusudio ya yale aliyoyapokea al-Bukhaariy na Muslim katika “as-Swahiyh” zao katika Hadiyth ya Mu´aawiyah na al-Mughiyrah bin Shu´bah waliosimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Halitoacha kundi katika Ummah wangu wenye kusimama juu ya amri ya Allaah. Hawatodhurika na wale wenye kwenda kinyume nao mpaka ifike amri ya Allaah.”

Amesema zaidi ya mwanachuoni mmoja: “Wakusudiwa ni Ahl-ul-Hadiyth kwa kuwa hawafanyi ushabiki kwa madhehebu yoyote. Wanafanya ushabiki kwa haki. Haitakikani kufupika kwa wale Muhaddithuun peke yao. Mtu mwema anayefuata haki ni katika kundi lililookoka (Firqat-un-Naajiyah) hata kama hatokuwa Muhaddith. Pamoja na kwamba wale Muhaddithuun wanashika nafasi ya mbele kabisa.”

Maneno ya Shaykh Muqbil (Rahimahu Allaah) yako wazi kwamba mtu mwema anayefuata haki ni katika Firqat-un-Naajiyah. Hakusema kuwa yuko karibu.

al-Hajuuriy anajaribu kuyapindisha[1] maneno haya ili yaweze kuafikiana na matamanio yake.

[1] al-Hajuuriy amesema katika mkanda “Tabyiyn al-Kadhib wal-Yamiyn”:

“Mtu huyu anasema kwamba sisi tunasema kuwa kundi lililo karibu zaidi na haki [ni Ahl-us-Sunnah]. Haya sio maneno yetu sisi tu. Haya ni maneno ya mwalimu wetu pia na yametajwa na yanajulikana kutoka kwake. Wanayajua wanafunzi wake watukufu na sio mtu kama wewe uliyeanguka.”

  • Mhusika: Shaykh ´Arafaat bin Hasan bin Ja´far al-Muhammadiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Bayaan al-Fawriy (01/19)
  • Imechapishwa: 11/10/2016