Mambo ya ndoa ya nchi za nje zinapelekwa kwenye vituo vya Kiislamu

Swali: Mwanamke anayeishi magharibini ameolewa ndoa ya Kishari´ah msikitini na kwa ndoa vilevile ya kiserikali mahakamani. Kisha mume wake akamtaliki talaka ya Kishari´ah kwa kuwepo mashahidi wawili bila ya kusajili talaka hii mahakamani. Je, inajuzu kwake kuolewa na mwanaume mwingine kwa ndoa ya Kishari´ah kabla ya kutimia talaka ya serikali mahakamani? Kwa sababu akizaa kwa huyu mume wa pili serikali itamnasibisha mtoto kwa yule mume wa kwanza kwa sababu ndio mwenye kutambulika serikalini.

Jibu: Mambo ya ndoa na talaka ya miji ya nje, ina vituo vyake vya Kiislamu huko. Aende kwenye kituo cha Kiislamu kilicho karibu na yeye na kitaangalia suala lake juu ya talaka na ndoa hiyo. Sisi hatujui kinachoendelea.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (57) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-01-07.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020