Katika hali ya mauti mali sio yako tena

Swali: Kuna mtu tajiri aliishi maisha yasiyokuwa ya kidini na akafa kwa sababu ya maradhi ya ukimwi. Kabla ya kufa kwake aliwakilisha mtu atoe swadaqah kwa mali zake zote kwa sababu warithi [wote] ni matajiri na ameona kuna haja ya kutoa kafara ya madhambi yake na kwamba hilo ni muhimu kuliko warithi wanavohitajia mali yake. Je, inajuzu kwa wakili kutekeleza wasia huu…

Jibu: Hapana, mali sio ya kwake. Mauti yakishamfika, bali akipatwa na maradhi ya mauti, mali zake zinamkimbia. Mali sio ya kwake tena. Itawaendea warithi. Hana haki ya kuiendesha atakavyo isipokuwa thuluthi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amempa rukhusa ya kutumia thuluthi na chini ya hapo tu. Mali ni ya warithi na sio ya kwake tena.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (57) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tf–1432-01-07.mp3
  • Imechapishwa: 21/08/2020