Mama, dada, msichana na mke wa mswaliji wanaruhusiwa kupita mbele yake?

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ametueleza kwamba kupita kwa mwanamke mbele ya anayeswali kunabatilisha swalah yake. Je, hili linawahusu pia mama, mke na dada?

Jibu: Hadiyth iliyotajwa ni yenye kuenea. Inamhusu mama, dada, msichana, mke na wengineo, kwa sababu hakuna dalili inayoonesha kuwa baadhi yao wametengwa katika hukumu hii.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (29/335)
  • Imechapishwa: 13/03/2026