Swali: Ni ipi hukumu ya kuunganisha uhusiano na mke wa baba ambaye tayari aliyemwacha? Je, inanilazimu kumtembelea ilihali mama yangu amenifungisha kiapo nisimtembelee? Nifanye nini?
Jibu: Huna wajibu wowote juu yako. Baba yako akishamwacha, yeye si katika jamaa zako wa damu na wala si miongoni mwa jamaa wa karibu. Yeye ni mke wa baba aliyeachwa tu. Ikiwa mama yako haridhii kumtembelea, basi usimtembelee. Yeye ni Mahram wako. Mke wa baba yako ambaye baba yako amemwacha au aliyefiwa naye, ni Mahram kwako kwa maafikiano ya waislamu. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
وَلَا تَنكِحُوا مَا نَكَحَ آبَاؤُكُم مِّنَ النِّسَاءِ
“Na wala msiwaoe [wake] waliowaoa baba zenu.” (04:22)
Lakini ikiwa utamzuru kwa minajili ya kumtendea wema na kwa kuzingatia haki ya baba yako, basi hilo ni jema. Ukimtembelea, ukamuheshimu au ukampa mali, hili ni katika maadili mema na katika mema yanayopendekezwa. Lakini muda wa kuwa jambo hilo linamghadhibisha mama yako na haliridhiiwi na mama yako, basi usifanye jambo linalomghadhibisha mama yako. Ikiwa utamfikia kwa njia ya siri bila mama yako kujua, basi hakuna tatizo.
Kwa kumalizia ni kwamba usimghadhibishe mama yako kwa njia hii. Hujalazimishwa kumtembelea wala kumfikia, kwa sababu si katika jamaa wa damu na wala si katika jamaa wa karibu. Yeye ni mke wa baba aliyeachwa au aliyefiwa naye. Kumfanyia wema ni katika maadili mema. Lakini usifanye hivyo ikiwa hilo litamdhuru au kumghadhibisha mama yako. Ukimfikia kwa siri pasi na mama yako kujua, basi hakuna tatizo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2130/حكم-صلة-زوجة-الاب-المطلقة
- Imechapishwa: 24/07/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya kuunganisha uhusiano na mke wa baba ambaye tayari aliyemwacha? Je, inanilazimu kumtembelea ilihali mama yangu amenifungisha kiapo nisimtembelee? Nifanye nini?
Jibu: Huna wajibu wowote juu yako. Baba yako akishamwacha, yeye si katika jamaa zako wa damu na wala si miongoni mwa jamaa wa karibu. Yeye ni mke wa baba aliyeachwa tu. Ikiwa mama yako haridhii kumtembelea, basi usimtembelee. Yeye ni Mahram wako. Mke wa baba yako ambaye baba yako amemwacha au aliyefiwa naye, ni Mahram kwako kwa maafikiano ya waislamu. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
وَلَا تَنكِحُوا مَا نَكَحَ آبَاؤُكُم مِّنَ النِّسَاءِ
“Na wala msiwaoe [wake] waliowaoa baba zenu.” (04:22)
Lakini ikiwa utamzuru kwa minajili ya kumtendea wema na kwa kuzingatia haki ya baba yako, basi hilo ni jema. Ukimtembelea, ukamuheshimu au ukampa mali, hili ni katika maadili mema na katika mema yanayopendekezwa. Lakini muda wa kuwa jambo hilo linamghadhibisha mama yako na haliridhiiwi na mama yako, basi usifanye jambo linalomghadhibisha mama yako. Ikiwa utamfikia kwa njia ya siri bila mama yako kujua, basi hakuna tatizo.
Kwa kumalizia ni kwamba usimghadhibishe mama yako kwa njia hii. Hujalazimishwa kumtembelea wala kumfikia, kwa sababu si katika jamaa wa damu na wala si katika jamaa wa karibu. Yeye ni mke wa baba aliyeachwa au aliyefiwa naye. Kumfanyia wema ni katika maadili mema. Lakini usifanye hivyo ikiwa hilo litamdhuru au kumghadhibisha mama yako. Ukimfikia kwa siri pasi na mama yako kujua, basi hakuna tatizo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2130/حكم-صلة-زوجة-الاب-المطلقة
Imechapishwa: 24/07/2026
https://firqatunnajia.com/mama-anakasirika-kwenda-kumtembelea-mke-wa-baba-aliyeachwa/