Swali: Ni ipi hukumu ya mtu anayefunga ndoa huku kwake yeye anaiona ndoa hiyo kuwa ya muda maalum pasi na mwanamke kujua kuwa ni ya muda maalum, khaswa ikiwa lengo lake ni kujilinda na maasi na katika hali yake ya sasa hawezi kuoa kwa namna ya kudumu?
Jibu: Ndoa ya Mut´ah ni batili kwa maafikiano ya waislamu. Haijuzu kabisa ndoay a Mut´ah. Ndoa ya Mut´ah ni ile ambayo mwanaume anamuoa mwanamke kwa sharti kwamba ataishi naye kwa muda maalum, kama mwezi mmoja, miwili au mitatu, kisha watengane na sharti hilo likiwa limewekwa wazi katika mkataba wa ndoa. Ndoa hii ilikuwa inajuzu mwanzoni mwa Uislamu, kisha ikafutwa na Allaah akaibatilisha na akaifanya kuwa haramu mpaka siku ya Qiyaamah. Hii ni miongoni mwa mambo yanayohalalishwa na baadhi ya Shiy´ah na Raafidhwah ambao huihalalisha ilihali ni jambo ovu katika matendo. Ikiwa mwanaume ataweka sharti kwa mwanamke au familia yake ikaweka sharti kwamba ndoa iwe ya miezi miwili, mitatu, mwaka mmoja au muda mwingine wowote na kwamba muda ukimalizika ndoa inaisha, basi hii ndiyo ndoa ya Mut´ah. Ndoa hii ni batili na ni maovu.
Ama ikiwa mwanaume atamuoa mwanamke bila kuweka sharti lolote, lakini moyoni mwake ana nia kwamba akimaliza masomo, kazi au ataondoka katika nchi hiyo, basi atampa talaka, basi maoni sahihi ni kwamba hii haihesabiwi kuwa ni ndoa ya Mut´ah. Nia iliyofichika moyoni haifanyi ndoa kuwa ya Mut´ah. Iwapo hakuna sharti lililowekwa baina yao, basi ndoa hiyo ni ndoa inayokubalika kwa mujibu wa Shari´ah. Huenda nia ikabadilika na huenda baadaye akaamua kuendelea naye kama mke wa kudumu. Nia hubadilika na hubadilishwa.
Kwa hiyo maoni sahihi ni kwamba ndoa ya Mut´ah haithibiti isipokuwa kwa kuweka sharti wazi katika mkataba wa ndoa. Ama nia iliyo moyoni bila sharti, haiathiri uhalali wa ndoa, ingawa kuna mitazamo tofauti kati ya wanazuoni katika suala hili.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2116/حكم-الزواج-الموقت-دون-اعلام-المراة
- Imechapishwa: 24/07/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya mtu anayefunga ndoa huku kwake yeye anaiona ndoa hiyo kuwa ya muda maalum pasi na mwanamke kujua kuwa ni ya muda maalum, khaswa ikiwa lengo lake ni kujilinda na maasi na katika hali yake ya sasa hawezi kuoa kwa namna ya kudumu?
Jibu: Ndoa ya Mut´ah ni batili kwa maafikiano ya waislamu. Haijuzu kabisa ndoay a Mut´ah. Ndoa ya Mut´ah ni ile ambayo mwanaume anamuoa mwanamke kwa sharti kwamba ataishi naye kwa muda maalum, kama mwezi mmoja, miwili au mitatu, kisha watengane na sharti hilo likiwa limewekwa wazi katika mkataba wa ndoa. Ndoa hii ilikuwa inajuzu mwanzoni mwa Uislamu, kisha ikafutwa na Allaah akaibatilisha na akaifanya kuwa haramu mpaka siku ya Qiyaamah. Hii ni miongoni mwa mambo yanayohalalishwa na baadhi ya Shiy´ah na Raafidhwah ambao huihalalisha ilihali ni jambo ovu katika matendo. Ikiwa mwanaume ataweka sharti kwa mwanamke au familia yake ikaweka sharti kwamba ndoa iwe ya miezi miwili, mitatu, mwaka mmoja au muda mwingine wowote na kwamba muda ukimalizika ndoa inaisha, basi hii ndiyo ndoa ya Mut´ah. Ndoa hii ni batili na ni maovu.
Ama ikiwa mwanaume atamuoa mwanamke bila kuweka sharti lolote, lakini moyoni mwake ana nia kwamba akimaliza masomo, kazi au ataondoka katika nchi hiyo, basi atampa talaka, basi maoni sahihi ni kwamba hii haihesabiwi kuwa ni ndoa ya Mut´ah. Nia iliyofichika moyoni haifanyi ndoa kuwa ya Mut´ah. Iwapo hakuna sharti lililowekwa baina yao, basi ndoa hiyo ni ndoa inayokubalika kwa mujibu wa Shari´ah. Huenda nia ikabadilika na huenda baadaye akaamua kuendelea naye kama mke wa kudumu. Nia hubadilika na hubadilishwa.
Kwa hiyo maoni sahihi ni kwamba ndoa ya Mut´ah haithibiti isipokuwa kwa kuweka sharti wazi katika mkataba wa ndoa. Ama nia iliyo moyoni bila sharti, haiathiri uhalali wa ndoa, ingawa kuna mitazamo tofauti kati ya wanazuoni katika suala hili.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2116/حكم-الزواج-الموقت-دون-اعلام-المراة
Imechapishwa: 24/07/2026
https://firqatunnajia.com/ibn-baaz-tofauti-ya-ndoa-ya-mutah-na-kuoa-kwa-nia-ya-kuacha/