Swali: Je, inajuzu kuoa wake zaidi ya mmoja ilihali kuna uwezo na uadilifu, bila kuwepo sababu nyingine ya juu zaidi isipokuwa tamaa ya kijinsia tu?
Jibu: Inajuzu sababu ya kuoa wake wengi ikawa ni kukidhi haja ya kijinsia, iwapo mke mmoja hamtoshelezi mume katika kujisitiri. Hakuna tatizo katika hilo. Bali huenda hata wake wawili wasimtimize, kwa kuwa watu wako katika aina na viwango tofauti. Kwa hiyo hakuna tatizo kuoa wake wawili, watatu au wanne pale panapohitajika na mume akijiona ana uwezo wa kutenda uadilifu na kutekeleza wajibu unaompasa. Hakuna ubaya katika hilo. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً
“Basi oeni waliokupendezeni katika wanawake wengine; wawili au watatu au wanne.”[1]
Hivyo ni lazima kwa mwanaume kuoa ili apate mke atakayemletea kukidhi haja ya kijinsia, utulivu na makazi ya nafsi, akiwa pamoja na mke wa kwanza, wa pili au wa tatu. Wa nne ndio mpaka wa mwisho.
[1] 04:03
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1974/حكم-الزواج-باكثر-من-واحدة-بنية-قضاء-الوطر
- Imechapishwa: 24/07/2026
Swali: Je, inajuzu kuoa wake zaidi ya mmoja ilihali kuna uwezo na uadilifu, bila kuwepo sababu nyingine ya juu zaidi isipokuwa tamaa ya kijinsia tu?
Jibu: Inajuzu sababu ya kuoa wake wengi ikawa ni kukidhi haja ya kijinsia, iwapo mke mmoja hamtoshelezi mume katika kujisitiri. Hakuna tatizo katika hilo. Bali huenda hata wake wawili wasimtimize, kwa kuwa watu wako katika aina na viwango tofauti. Kwa hiyo hakuna tatizo kuoa wake wawili, watatu au wanne pale panapohitajika na mume akijiona ana uwezo wa kutenda uadilifu na kutekeleza wajibu unaompasa. Hakuna ubaya katika hilo. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
فَانكِحُوا مَا طَابَ لَكُم مِّنَ النِّسَاءِ مَثْنَىٰ وَثُلَاثَ وَرُبَاعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُوا فَوَاحِدَةً
“Basi oeni waliokupendezeni katika wanawake wengine; wawili au watatu au wanne.”[1]
Hivyo ni lazima kwa mwanaume kuoa ili apate mke atakayemletea kukidhi haja ya kijinsia, utulivu na makazi ya nafsi, akiwa pamoja na mke wa kwanza, wa pili au wa tatu. Wa nne ndio mpaka wa mwisho.
[1] 04:03
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1974/حكم-الزواج-باكثر-من-واحدة-بنية-قضاء-الوطر
Imechapishwa: 24/07/2026
https://firqatunnajia.com/kuoa-mke-zaidi-ya-mmoja-kwa-lengo-la-kukidhi-tamaa-ya-kijinsia/