Swali: Mwanamke anawajibika na hukumu za Kishari´ah kuanzia umri gani?
Jibu: Mwanamke ni kama mwanaume. Mwanamke anawajibika kama mwanaume. Anawajibika kwa mambo matatu, na yeye mwanamke anaongezewa jambo la nne. Anapofikisha miaka kumi na tano na akaikamilisha, basi anakuwa mwanamke anayewajibika kwa swalah, swawm, hijjah na ´ibaadah nyenginezo. Pia akimea nywele sehemu ya siri, basi anakuwa anawajibika pia kama mwanaume. Vivyo hivyo kwa kutoka kwa manii, anapotoa manii kwa matamanio kwa sababu ya kuangalia, kufikiri au kwa kuota usingizini, basi kwa hilo anakuwa anawajibika kama mwanaume. Mambo haya matatu ni ya pamoja kati ya wanaume na wanawake.
1 – Kufikisha miaka kumi na tano kwa mujibu wa maoni yenye nguvu zaidi. Anapokamilisha miaka kumi na tano, basi anakuwa mwanamke anayewajibika kwa hukumu za dini kama mwanaume.
2 – Kumea kwa nywele zenye kuzunguka tupu ya mbele. Hili pia ni miongoni mwa sababu za kuwajibika kwa mwanaume na mwanamke wote wawili.
3 – Kutoka kwa manii kwa matamanio, ni mamoja iwe kwa kuota usingizini, kwa kufikiri, kuangalia na mfano wa hayo. Basi anapomwaga manii, basi wote wawili wanakuwa wanawajibika.
4 – Ni maalum kwake mwanamke, nalo ni hedhi. Anapopata hedhi, basi anakuwa amewajibika kwa hilo.
Haya ndiyo mambo ambayo kwayo kuna kuwajibika kwa mwanamke na mwanaume wote wawili. Matatu ni ya pamoja na la nne ni la mwanamke pekee, nalo ni hedhi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1941/وقت-تكليف-المراة-بالاحكام-الشرعية
- Imechapishwa: 24/07/2026
Swali: Mwanamke anawajibika na hukumu za Kishari´ah kuanzia umri gani?
Jibu: Mwanamke ni kama mwanaume. Mwanamke anawajibika kama mwanaume. Anawajibika kwa mambo matatu, na yeye mwanamke anaongezewa jambo la nne. Anapofikisha miaka kumi na tano na akaikamilisha, basi anakuwa mwanamke anayewajibika kwa swalah, swawm, hijjah na ´ibaadah nyenginezo. Pia akimea nywele sehemu ya siri, basi anakuwa anawajibika pia kama mwanaume. Vivyo hivyo kwa kutoka kwa manii, anapotoa manii kwa matamanio kwa sababu ya kuangalia, kufikiri au kwa kuota usingizini, basi kwa hilo anakuwa anawajibika kama mwanaume. Mambo haya matatu ni ya pamoja kati ya wanaume na wanawake.
1 – Kufikisha miaka kumi na tano kwa mujibu wa maoni yenye nguvu zaidi. Anapokamilisha miaka kumi na tano, basi anakuwa mwanamke anayewajibika kwa hukumu za dini kama mwanaume.
2 – Kumea kwa nywele zenye kuzunguka tupu ya mbele. Hili pia ni miongoni mwa sababu za kuwajibika kwa mwanaume na mwanamke wote wawili.
3 – Kutoka kwa manii kwa matamanio, ni mamoja iwe kwa kuota usingizini, kwa kufikiri, kuangalia na mfano wa hayo. Basi anapomwaga manii, basi wote wawili wanakuwa wanawajibika.
4 – Ni maalum kwake mwanamke, nalo ni hedhi. Anapopata hedhi, basi anakuwa amewajibika kwa hilo.
Haya ndiyo mambo ambayo kwayo kuna kuwajibika kwa mwanamke na mwanaume wote wawili. Matatu ni ya pamoja na la nne ni la mwanamke pekee, nalo ni hedhi.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1941/وقت-تكليف-المراة-بالاحكام-الشرعية
Imechapishwa: 24/07/2026
https://firqatunnajia.com/lini-mwanamke-anaanza-kuwajibika-na-hukumu-za-kidini/