Swali: Haifichiki kwenu kwamba benki zilizopo sasa ni benki za ribaa na zinashughulika na ribaa ndani ya Saudi Arabia na nje yake. Zimeweka sehemu ya mtaji wake kwa raia kama ushiriki na kwa mujibu wa wanavyojua baadhi ya watu kwamba ni halali. Basi juu yenu mbele ya Allaah mueleze hilo ili watu wawe juu ya bayana katika jambo hili. Kwa kuwa kila mtu anayetaka bidhaa kutoka nje haiji isipokuwa kupitia benki zilizopo. Kwa nini kusiwepo benki za Kiislamu zinazofanya hivyo?
Jibu: Benki za ribaa zote ni haramu na wajibu ni kutojihusisha nazo. Bali wajibu ni kuziepuka na kutojihusisha nazo, kwa sababu kushughulika nazo ni kusaidiana katika dhambi na uadui. Tumekwishaeleza jambo hili mara nyingi katika magazeti ya kitaifa na wengine pia wameeleza. Ufafanuzi wa uharamu wa ribaa uko wazi katika Qur-aan na Sunnah.
Hakuna shaka kwamba onyo letu dhidi ya ribaa ni wajibu. Basi wanazuoni wanapaswa kuonya dhidi ya ribaa daima, kuwabainishia watu kwamba ni katika madhambi makubwa, kwamba ni khatari kubwa na ni miongoni mwa sababu za adhabu za jumla. Kuenea kwa ribaa, zinaa, ulevi, kusengenya, umbea, kuasi wazazi, kukata undugu na mfano wa hayo katika maasi yote ni miongoni mwa sababu za adhabu za jumla. Kwa hiyo ni wajibu kujihadhari na hilo na wajibu juu ya kila muislamu ni kujihadhari na hilo.
Tunamuomba Allaah aifanye iwe rahisi kupatikana benki za Kiislamu karibuni. Kwa hakika dola – Allaah aiwezeshe – imeahidi jambo hili, la kupatikana benki za Kiislamu, na kuwepo taasisi za Kiislamu zitakazotosheleza badala ya benki za ribaa. Na tunatarajia jambo hili lianze karibuni – Allaah akitaka – ili ziondolewe benki hizi za ribaa, au Allaah awaongoe, warejee kwenye usahihi.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1922/البنوك-الربوية-وخطرها-والتحذير-منها
- Imechapishwa: 24/07/2026
Swali: Haifichiki kwenu kwamba benki zilizopo sasa ni benki za ribaa na zinashughulika na ribaa ndani ya Saudi Arabia na nje yake. Zimeweka sehemu ya mtaji wake kwa raia kama ushiriki na kwa mujibu wa wanavyojua baadhi ya watu kwamba ni halali. Basi juu yenu mbele ya Allaah mueleze hilo ili watu wawe juu ya bayana katika jambo hili. Kwa kuwa kila mtu anayetaka bidhaa kutoka nje haiji isipokuwa kupitia benki zilizopo. Kwa nini kusiwepo benki za Kiislamu zinazofanya hivyo?
Jibu: Benki za ribaa zote ni haramu na wajibu ni kutojihusisha nazo. Bali wajibu ni kuziepuka na kutojihusisha nazo, kwa sababu kushughulika nazo ni kusaidiana katika dhambi na uadui. Tumekwishaeleza jambo hili mara nyingi katika magazeti ya kitaifa na wengine pia wameeleza. Ufafanuzi wa uharamu wa ribaa uko wazi katika Qur-aan na Sunnah.
Hakuna shaka kwamba onyo letu dhidi ya ribaa ni wajibu. Basi wanazuoni wanapaswa kuonya dhidi ya ribaa daima, kuwabainishia watu kwamba ni katika madhambi makubwa, kwamba ni khatari kubwa na ni miongoni mwa sababu za adhabu za jumla. Kuenea kwa ribaa, zinaa, ulevi, kusengenya, umbea, kuasi wazazi, kukata undugu na mfano wa hayo katika maasi yote ni miongoni mwa sababu za adhabu za jumla. Kwa hiyo ni wajibu kujihadhari na hilo na wajibu juu ya kila muislamu ni kujihadhari na hilo.
Tunamuomba Allaah aifanye iwe rahisi kupatikana benki za Kiislamu karibuni. Kwa hakika dola – Allaah aiwezeshe – imeahidi jambo hili, la kupatikana benki za Kiislamu, na kuwepo taasisi za Kiislamu zitakazotosheleza badala ya benki za ribaa. Na tunatarajia jambo hili lianze karibuni – Allaah akitaka – ili ziondolewe benki hizi za ribaa, au Allaah awaongoe, warejee kwenye usahihi.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1922/البنوك-الربوية-وخطرها-والتحذير-منها
Imechapishwa: 24/07/2026
https://firqatunnajia.com/matahadharisho-juu-ya-benki-za-ribaa/