Hakika moto huu tunaotumiwa hapa duniani ni sehemu katika sehemu sitini za Moto wa Jahannam. Kila moto wa duniani, mkali na khafifu, ni sehemu katika sehemu sitina za Moto wa Jahannam. Allaah atuepushe nao sisi na nyinyi. Allaah ameufanya kuwa ni ukumbusho[1]. Baadhi ya Salaf walipokuwa wakitamani kufanya maasi, wanaenda kwenye moto na kuweka kidole chake juu yake. Kwa msemo mwingine anajiambia nafsi yake “Kumbuka ukali huu ili usiende kufanya maasi ambayo ni sababu ya kuingia Motoni.” Tunamuomba Allaah afya.

[1] Waaqi´ah 56:71-72

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/291)
  • Imechapishwa: 27/09/2024