Makusudio ya Ahl-us-Sunnah wanaposema “Hawakufurishi kwa madhambi”

Kuzidi na kupungua kwa imani ni msingi kwa Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah wanaotofautiana kwao na Khawaarij na kila mwenye kukafirisha kwa madhambi.

Ahl-us-Sunnah wanasema kuwa hawakufurishi kwa madhambi. Wanachokusudia ni kwamba hawakufurishi kwa kutenda maasi. Ama kuhusu kukufurisha juu ya nguzo za Uislamu kubwa; swalah, zakaah na hajj kuna tofauti inayojulikana. Kwa hivyo msemo wao kwamba Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah hawakufurishi kwa dhambi midhali mtu haihalalishi na kwamba haya ni kwa maafikiano, wanachomaanisha ni maasi. Kuhusu ile misingi mikubwa kuna tofauti inayojulikana walionayo. Kuna ambao wanakufurisha kwa kuacha misingi hiyo mikubwa au kuacha msingi moja wapo katika hiyo na kuna wengine ambao hawakufurishi.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 111-112
  • Imechapishwa: 27/08/2020