Jabriyyah wamegawanyika sehemu mbili:

1- Jabriyyah waliopindukia: Hawa ni wale wanaosema kuwa mwanaadamu hana khiyari kabisa. Wanasema ni kama bendera yenye kuendeshwa na upepo. Hii ndio I´tiqaad ya Jahmiyyah na kundi katika Suufiyyah waliopundukia. Wanapatikana leo.

2- Jabriyyah ambao hawakupindukia: Hawa ni Ashaa´irah. Hakika Ashaa´irah wanazungumza kwa I´tiqaad ya Jabriyyah, lakini hata hivyo ni madhehebu ya Jabriyyah ya ndani na sio ya dhahiri. Wanasema kwamba udhahiri wa mja ni kwamba ni mwenye khiyari, lakini uhakika wa mambo ni kwamba ametenzwa nguvu kwa ndani. Kwa ajili hii ndio maana wakazua tamko la ´kuchuma`. Wamesema kuwa matendo ni chumo la mja. Nini maana yake? Viongozi wao wametofautiana juu ya kufasiri neno ´chumo` katika maoni kumi na moja. Hatuna nafasi ya kutaja maoni haya hapa. Lakini kwa ufupi wanachotaka ni kwamba hawaonelei kama kuna maana yoyote ya kuchuma/kutenda.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Lum´at-il-I´tiqaad, uk. 99-100
  • Imechapishwa: 27/08/2020