Makampuni ya Ulaya yasiyowaruhusu waajiri kwenda kuswali ijumaa msikitini

Swali: Baadhi ya taasisi huko Ulaya hazimruhusu muislamu kuacha kazi kwa ajili ya kuswali ijumaa?

Jibu: Hali hii ni kama mlinzi. Ikiwa haruhusiwi, basi hili ni udhuru kwake. Ni kama mlinzi anayelinda nyumba, gereza au mali. Ni udhuru kwake kuswali Dhuhr ikiwa hawezi kuhudhuria swalah ya ijumaa. Ni kama mgonjwa ambaye anakuwa na udhuru. Anapewa udhuru wa kuacha wa kuacha ijumaa msikitini ikiwa hawezi kufika kwa sababu ya kuwa mlinzi, mgonjwa, mwenye khofu au hali kama hizo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/25152/حكم-من-يمنعه-عمله-عن-اداء-صلاة-الجمعة
  • Imechapishwa: 08/02/2025