Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakuna yeyote atayesikia kuhusu kuja kwangu, si myahudi wala mkristo, kisha akafariki bila ya kuamini dini niliyotumwa nayo, isipokuwa atakuwa katika watu wa Motoni.”[1]

Tunaamini na kuitakidi kuwa manaswara, mayahudi na makafiri wengine wote ya kuwa ni katika watu wa Motoni. Namna hii ndivyo alivyoshuhudia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Wamekufuru. Ni maadui wa Allaah. Ni maadui wa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam); Ibraahiym, Nuuh, Muhammad, Muusa, ´Iysaa na Mitume wengine wote (´alayhimus-Salaam).

[1] Muslim (153).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (01/350)
  • Imechapishwa: 04/05/2023